Posts

Darasa Kiganjani.........Njia tofauti za kufuga kuku. Faida zake Na Hasara Zake

Image
Mambo yanayomfanya mfugaji kuamua atumie njia fulani ya kufuga ni pamoja na uwezo wa kugharamia shughuli ya ufugaji wa kuku na ukubwa wa eneo alilonalo la kufugia. Katika sehemu hii utajifunza njia tatu za kufuga kuku ambazo ni:  1. Kufuga huria Kuku huachwa wenyewe kujitafutia chakula na maji. Njia hii inatumika zaidi kufuga kuku wa kienyeji. Mara chache sana mfugaji huwapatia kuku chakula cha ziada. Kwa ufugaji huu lazima kuwe na eneo kubwa la kutosha kuku kuzunguka na kutafuta chakula. Kuku hulala eneo lisilo rasmi kama vile jikoni, kwenye kiambata n.k. Faida zake  • Ni njia rahisi ya kufuga.  • Gharama yake pia ni ndogo.  • Kuku wanapata mazoezi ya kutosha.  • Kuku wanapata chakula mchanganyiko ambacho kinafaa kiafya.  Hasara zake  • Kuku huwa hatarini kuibiwa au kudhurika na wanyama wakali na hali mbaya ya hewa. • Ukuaji wa kuku ni hafifu, hufikia uzito wa kilo 1.2 baada ya mwaka. • Huharibu mazingira kama kula na mime...

Darasa Kiganjani-------Aina ya chanjo Kwa Kuku na Namna ya Kuchanja!!!

Je, una ufahamu kuwa chanjo ni kwa ajili ya kuzuia magonjwa mbalimbali yasiwadhuru kuku wako hivyo hupewa kwa kuku Wenye afya tu ambao sio wagonjwa? Na kuwa Chanjo zipo za aina kuu 2? Basi twende Pamoja!! Aina za Chanjo 1.Chanjo zilizo hai /live Virus vaccines Hizi ni chanjo zenye virusi Hai kwa ajili ya kinga dhidi ya ugonjwa fulani na ni lazima vifike mwilini vikiwa hivyo hivyo hai. *Sifa*kuu ya chanjo hizi ni kuwa kinga yake hukaa kwa muda mfupi mwilini na ndizo chanjo za awali mfano ni chanjo ya Newcastle na Gumboro. 2.Chanjo zisizo na uhai dead vaccines Hizi ni chanjo zenye virusi visivyo na uhai /vimekufa. *Aina za Chanjo kulingana na umri wa kuku* *Siku ya 1*: MAREK'S /MAHEPE. Chanjo hii hupewa kifaranga wa siku 1mara tu ya kuanguliwa na kinga hudumu kwa maisha yake yote, mara nyingi hutolewa hatchery kwenye makampuni yanayototolesha vifaranga ingawa baadhi ya makampuni hudanganya wafugaji kuwa wamechanjwa wakati hawakuchanjwa ila kwa kujiridhisha zaidi ...