Posts

Showing posts from April 9, 2017

Ulezi Bora Wa Vifaranga huleta Matokeo Bora Kwenye Mradi wa Kuku!!

Image
Malezi bora ya vifaranga ni muhimu katika ufugaji wa kuku kwa sababu vifaranga hawana uwezo wa kustahimili mazingira wakiwa wenyewe mara wanapoanguliwa.Ukosefu wa malezi bora husababisha vifaranga kuwa dhaifu,kufa kwa wingi na hivyo kupunguza idadi ya kuku wa baadaye. Malezi ya vifaranga yanaweza kufanyika kwa kutumia kuku walezi au kutumia vifaa maalum. KULEA VIFARANGA KWA KUTUMIA KUKU MLEZI Vifaranga wanaweza kulelewa na mama yao au kuku mlezi. Endapo kuku wengi wametotoa vifaranga kwa wakati mmoja, achaguliwe kuku mlezi aliye na uwezo wa kulea vifaranga wengi kati ya waliototoa aendelee kulea na wengine waliototoa waachwe huru ili warudi kwenye mzunguko wa kutaga. Kuku mmoja anaweza kulea vifaranga 20 hadi 25. Mfugaji wa kuku,pamoja na kanuni nyingine, anapaswa kuzingatia yafuatayo:-  • Kuku anayelea vifaranga atengewe chumba maalumu, apewe maji ya kutosha na chakula chenye virutubisho muhimu,  • Vifaranga wasiachiwe kutoka nje hadi watakapofika umri wa wiki ...