Posts

Showing posts from April 2, 2017

Bora Kinga Kwa Kuku Kuliko Tiba!!!Usithubutu kusubiri Tiba.

Image
Kinga ni bora zaidi kwani ndio namna pekeee ya kuweza kuwaokoa kuku wako kwasababu magonjwa mengi hayana tiba hivyo ili kwenda sawa na kunufaika na mradi wako basi fuata ratiba hii ya chanjo kwa kuku wako!!! 1. SIKU 1. Baada ya vifaranga kutotoreshwa wenye siku moja,vifranga wapewe glucose kwa muda wa masaa 2.Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa.baada ya hapo vifaranga wapewe vitamin mfano ni CHAMPRIX.Pia hii huchanganywa na maji.vifaranga wawe katika eneo lenye joto na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifanga wapewe OTC plus(kijiko kimoja cha chai katika lita 5 za maji safi,pia changanya vitamin. Chanjo-Marek´s 2. SIKU YA 7 . vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDELI).chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kasha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye vitamin. ...

Mwongozo kwa mfugaji wa kuku wa kienyeji,ila utafiti wa eneo lako ni muhimu sana!!

Pengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo. Somo langu ni dogo lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana. Sasa kuwa makini zaidi. Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo. Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4 .  Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa makoo(majike) watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 6-7 au zaidi nao wataanza kutaga. Utakuwa na kuku 200 + 25 =225 ndani ya miezi 14. Miezi 7 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700.  hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa miezi 24(miak...

Mchango wa Mazingira Kwa Ulaji wa Kuku!!

Image
Kuna sababu mbalimbali zinazoathiri ulaji wa kuku, athari hizo zinaweza zikamfanya kuku ale sana au asile kabisa. Zifuatazo ni sababu za kimazingira zinazoathiri ulaji wa kuku:- JOTO Ulaji wa chakula hupungua kadri joto la mazingira linavyoongezeka, kwan kama tujuavyo zoezi la umeng'enyaji wa chakula huongeza joto la mwili, na joto la mwili halitakiwi kupanda wala kupungua, hivyo basi ubongo unamuamuru kuku asile ili kudhibiti joto la mwili lisipande. Angalizo ni kwamba mfugaji anatakiwa achunge hali ya joto la banda, kwan hata akizidisha balbu au banda likikosa hewa ya kutosha pia inaweza kusababisha joto la mazingira kuongezeka na kupelekea kuku kukosa hamu ya kula hali amabayo itawafanya kuku wadumae.  BARIDI Kipindi cha baridi kuku wanakula sana kwa sababu ubongo unamuamuru kuku ale sana kwa kuwa umeng'enyaji unatakiwa uwe mara kwa mara ili kudhibiti joto la mwili lisishuke.  Msongo Banda likiwa chafu, au lipo sehemu yenye kelele za mara kwa ma...

Ushauri Kwa Mfugaji Wa Kuku Mpya

Image
Hii ni kwa wote, wafugaji na wanaotaka kuanza kufuga. Unapotaka kuanza ufugaji unatakiwa uanze na ufugaji mdogo hatakama una mtaji mkubwa. Kwa kufanya hivi itakusaidia kupata uzoefu katika nyajna zifuatazo: UTUNZAJI Kwa kuanza na kiasi kidogo itakusaidia kujua ni ukubwa gani unafaa kwa kuku wangapi, ukiwa na kuku wangapi utalisha chakula kiasi gani, pia utapata uzoefu wa chanjo muhimu zinazohitajika hali ambayo itakurahisishia pindi utapoanza ufugaji mkubwa. SOKO Hapa tunalenga upatikanaji wa wateja wa bidhaa zako za mifugo, itakusaidia kujua wateja waliopo wanavutiwa na bidhaa ya aina gani, kwa mfano mayai utajua wanapenda mayai ya kiini cheupe au cha njano? Kwa kufaham wanchokihitaji utajua ufanye nini ili ukidhi wanachokihitaji. CHANGAMOTO Ukianza na ufugaji mdogo pia itakusaidia kujua changamoto zilizopo kwenye ufugaji na utajifunza ni jinsi gani ya kuzitatua au kukabiliananazo kabla  ya kuanza ufugaji mkubwa.

Uchambuzi Makini wa Ugonjwa Wa MDONDO/KIDERI Kwa Kuku- NEWCASTLE DISEASE.

Image
Ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege ambao unasababishwa na vimelea aina ya paramyxovirus. Kuenea kwa UgonjwaUgonjwa wa Mdondo (Newcastle disease) huenea kupitia njia mbalimbali kama zifuatazo:- Mayai ya kuku aliyeugua ugonjwa wa mdondo/kideri (Newcastle disease). Kugusana na kuku mgonjwa. Kupitia maji yenye maambukizi. Wakati wa totoleshaji vifaranga. Chakula chenye maambukizi. Hewa yenye maambukizi ya ugonjwa huu. Dalili za Mdondo/Kideri (Newcastle disease) Vifo vya ghafla. 2. Kutoa udenda mdomoni. 3. Kukosa hamu ya kula. 4. Kuharisha kinyesi cheupe na kijani. 5. Kuhema kwa shida. 6. Kukakamaa viungo au kupooza hasa mabawa, shingo na miguu. 7. Kupunguza utagaji. 8. Vifo hutegemea kasi ya ugonjwa huweza kufikia hadi asilimia mia moja (100%). Namna ya kudhibiti Mdondo/Kideri (Newcastle disease) Wapewe chanjo kwa muda unaofaa (Siku ya 7 na 28, na kila baada ya miezi 3). Kuku wote walioz...

DONDOO YA KUANZA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KAMA MRADI

Image
MAHITAJI Kuku(tetea) 10 na Jogoo 01 Banda bora Vyombo vya chakula na maji Chakula bora Madawa na chanjo kwajili ya magonjwa Chanzo cha nishati joto na mwanga Elimu na ujuzi wa malezi bora Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa) Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu KUKU 10 Wakati wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 10 (matetea) wenye umri sawa na hawajawai kutaga hata mara moja. Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika familia bora kutegemea malengo ya mradi wako. Mfano kama lengo lako ni kuzalisha kuku wa kienyeji kwajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa haraka na yenye uzito mkubwa. Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi. Ili kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao. Kuku hawa utawapata kwa bei ya chini, tena wataf...

UJENZI WA BANDA BORA LA KUKU

Mfugaji anaweza kudhani kuwa mradi wa kuku unaweza kumpatia faida kubwa bila kujali uwepo wa banda zuri na imara. Banda lililojengwa imara hudhibiti maadui wa kuku na kufanya uzalishaji kuwa bora zaidi.  Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ujenzi wa banda: 1.Idadi Ya Kuku Idadi ya kuku Kabla ya kuanza kujenga banda, mfugaji anatakiwa kujua kuwa anataka kufuga kuku wa aina gani na wangapi. Hii itamwezesha mfugaji kujua ukubwa wa banda linalohitajika. 2. Uwezo wa Mfugaji Kifedha. Ujenzi wa banda unahitaji fedha nyingi kama ni ufugaji wa kuku wengi,hivyo ni lazima mfugaji ajue kuwa banda analotaka kujenga atalimaliza kwa kuangalia bajeti iliyopo mezani kwa ajili ya kazi hiyo. 3 . Eneo la kujenga banda. Mfugaji lazima awe na eneo la kujenga banda na liwe na sifa zifuatazo:- Mwinuko - Iwe sehemu iliyoinuka isiyotuamisha maji kirahisi. Eneo lisiwe mbali na sehemu ya kuishi ili kuweza kulinda. Uwezekano wa Upanuzi - Sehemu iwe pana na kubwa ...

MAGONJWA YA KUKU

Image
Mdondo/New castle Virus vinavyosababisha ugonjwa huu huenezwa kwa hewa Dalili Kuhalisha choo cha kijani na njano Kukohoa na kupumua kwa shida Kupinda shingo kwa nyuma Kuficha kichwa katikati ya miguu Kukosa hamu ya kula na kunywa Idadi kubwa ya vifo hadi 90% Kinga Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3 Epuka kuingiza kuku wageni Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa Zingatia usafi wa mazingira NDUI YA KUKU/ FOWL POX Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu Dalili Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana Kukosa hamu ya kula Vifo vingi Kinga Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine Epuka kuingiza kuku wageni Zingatia usafi wa mazingira HOMA YA MATUMBO/FOWL TYPHOID Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe Kuku hukosa hamu ya kula Kuku hukonda Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu Kinyeshi hushikam...

Mfahamu Kuku KIBiolojia

Image
Kuku hutegemea mimea, wadudu na wanyama wadogo wadogo kama chakula (omnivores), na ndio maana mara nyingi hufukua chini ardhini kutafuta wadudu na wanyama wadogo kama panya wadogo, vimjusi vidogodogo na hukata sehemu changa za mimea ambazo ni laini kwa mlo. Kuku huweza kuishi hadi miaka mitano hadi kumi,japo hii hutegemea mambo mengi ikiwepo hali ya hewa,chakula na pia aina ya mbegu ya kuku husika. Kuku aliyeripotiwa kusihi miaka mingi aliishi miaka kumi na sita (Jarida la Rekodi duniani la Guinnes),kuku huyo alikufa baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi. Ni rahisi sana kumtofautisha jogoo na mtetea kutokana na maumbo yao tofauti hata wakiwa wadogo kwani Jogoo huwa na manyoya menhi mkiani ukilinganisha na ya mtetea pia sehemu ya kichwa chake juu (comb) huwa ndefu na chini ya kidevu (wattles), manyoya mengi shingoni licha ya kwamba wanatokana na mbegu moja. Ndege hawa wa nyumbani hawana uwezo wa kuruka na kupaa mbali bali huruka umbali mfupi tu kuruka uzio au kupanda j...