Ushauri Kwa Mfugaji Wa Kuku Mpya

Hii ni kwa wote, wafugaji na wanaotaka kuanza kufuga. Unapotaka kuanza ufugaji unatakiwa uanze na ufugaji mdogo hatakama una mtaji mkubwa. Kwa kufanya hivi itakusaidia kupata uzoefu katika nyajna zifuatazo:


UTUNZAJI
Kwa kuanza na kiasi kidogo itakusaidia kujua ni ukubwa gani unafaa kwa kuku wangapi, ukiwa na kuku wangapi utalisha chakula kiasi gani, pia utapata uzoefu wa chanjo muhimu zinazohitajika hali ambayo itakurahisishia pindi utapoanza ufugaji mkubwa.



SOKO
Hapa tunalenga upatikanaji wa wateja wa bidhaa zako za mifugo, itakusaidia kujua wateja waliopo wanavutiwa na bidhaa ya aina gani, kwa mfano mayai utajua wanapenda mayai ya kiini cheupe au cha njano? Kwa kufaham wanchokihitaji utajua ufanye nini ili ukidhi wanachokihitaji.



CHANGAMOTO
Ukianza na ufugaji mdogo pia itakusaidia kujua changamoto zilizopo kwenye ufugaji na utajifunza ni jinsi gani ya kuzitatua au kukabiliananazo kabla  ya kuanza ufugaji mkubwa.

Comments

Popular posts from this blog

Darasa Kiganjani-------Aina ya chanjo Kwa Kuku na Namna ya Kuchanja!!!

Ufugaji Wa kuku wa Kienyeji Kitaalamu-Mambo (6) ya Kuzingatia

Uchambuzi Makini wa Ugonjwa Wa MDONDO/KIDERI Kwa Kuku- NEWCASTLE DISEASE.