Darasa Kiganjani.........Njia tofauti za kufuga kuku. Faida zake Na Hasara Zake
Mambo yanayomfanya mfugaji kuamua atumie njia fulani ya kufuga ni pamoja na uwezo wa kugharamia shughuli ya ufugaji wa kuku na ukubwa wa eneo alilonalo la kufugia. Katika sehemu hii utajifunza njia tatu za kufuga kuku ambazo ni: 1. Kufuga huria Kuku huachwa wenyewe kujitafutia chakula na maji. Njia hii inatumika zaidi kufuga kuku wa kienyeji. Mara chache sana mfugaji huwapatia kuku chakula cha ziada. Kwa ufugaji huu lazima kuwe na eneo kubwa la kutosha kuku kuzunguka na kutafuta chakula. Kuku hulala eneo lisilo rasmi kama vile jikoni, kwenye kiambata n.k. Faida zake • Ni njia rahisi ya kufuga. • Gharama yake pia ni ndogo. • Kuku wanapata mazoezi ya kutosha. • Kuku wanapata chakula mchanganyiko ambacho kinafaa kiafya. Hasara zake • Kuku huwa hatarini kuibiwa au kudhurika na wanyama wakali na hali mbaya ya hewa. • Ukuaji wa kuku ni hafifu, hufikia uzito wa kilo 1.2 baada ya mwaka. • Huharibu mazingira kama kula na mime...