Mfahamu Kuku KIBiolojia
Kuku hutegemea mimea, wadudu na wanyama wadogo wadogo kama chakula (omnivores), na ndio maana mara nyingi hufukua chini ardhini kutafuta wadudu na wanyama wadogo kama panya wadogo, vimjusi vidogodogo na hukata sehemu changa za mimea ambazo ni laini kwa mlo.
Kuku huweza kuishi hadi miaka mitano hadi kumi,japo hii hutegemea mambo mengi ikiwepo hali ya hewa,chakula na pia aina ya mbegu ya kuku husika. Kuku aliyeripotiwa kusihi miaka mingi aliishi miaka kumi na sita (Jarida la Rekodi duniani la Guinnes),kuku huyo alikufa baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi.
Ni rahisi sana kumtofautisha jogoo na mtetea kutokana na maumbo yao tofauti hata wakiwa wadogo kwani Jogoo huwa na manyoya menhi mkiani ukilinganisha na ya mtetea pia sehemu ya kichwa chake juu (comb) huwa ndefu na chini ya kidevu (wattles), manyoya mengi shingoni licha ya kwamba wanatokana na mbegu moja.
Ndege hawa wa nyumbani hawana uwezo wa kuruka na kupaa mbali bali huruka umbali mfupi tu kuruka uzio au kupanda juu ya mti ulio chini ili kupumzima au kuwika kwa majogoo. Mara nyingi kuku hupaa kuongea uwezo wao wa kukimbia lwa haraka pale wanapohisi kuna hatari inayowakaribia.
Comments