Ulezi Bora Wa Vifaranga huleta Matokeo Bora Kwenye Mradi wa Kuku!!
Malezi bora ya vifaranga ni muhimu katika ufugaji wa kuku kwa sababu vifaranga hawana uwezo wa kustahimili mazingira wakiwa wenyewe mara wanapoanguliwa.Ukosefu wa malezi bora husababisha vifaranga kuwa dhaifu,kufa kwa wingi na hivyo kupunguza idadi ya kuku wa baadaye. Malezi ya vifaranga yanaweza kufanyika kwa kutumia kuku walezi au kutumia vifaa maalum.
KULEA VIFARANGA KWA KUTUMIA KUKU MLEZI
Vifaranga wanaweza kulelewa na mama yao au kuku mlezi. Endapo kuku wengi wametotoa vifaranga kwa wakati mmoja, achaguliwe kuku mlezi aliye na uwezo wa kulea vifaranga wengi kati ya waliototoa aendelee kulea na wengine waliototoa waachwe huru ili warudi kwenye mzunguko wa kutaga. Kuku mmoja anaweza kulea vifaranga 20 hadi 25. Mfugaji wa kuku,pamoja na kanuni nyingine, anapaswa kuzingatia yafuatayo:-
• Kuku anayelea vifaranga atengewe chumba maalumu, apewe maji ya kutosha na chakula chenye virutubisho muhimu,
• Vifaranga wasiachiwe kutoka nje hadi watakapofika umri wa wiki 6,
• Vifaranga watengwe na mama/mlezi baada ya wiki 4 kuruhusu mama aendelee na mzunguko wa kutaga;na
• Katika maeneo yenye hali ya hewa ya ubaridi vifaranga wacheleweshwe kutenganishwa na mama/mlezi hadi wiki ya 6 au mpaka waonekane wameota manyoya ya kutosha.
KULEA VIFARANGA KWA KUTUMIA BRUDA
Bruda ni chombo/sehemu iliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwapatia joto vifaranga badala ya mama/mlezi. Mfugaji anaweza kulea vifaranga wengi kwa kutumia bruda ambayo ni mduara unaweza kutengenezwa kwa kutumia mbao, karatasi ngumu au kwa kuziba pembe za chumba.Aidha, njia hii hupunguza vifo vya vifaranga vinavyosababishwa na ndege au wanyama hatari,huruhusu kuku kutaga mapema zaidi na kuwa na mizunguko mingi ya utagaji (kwa kuku wanaoatamia). Vilevile, hurahisisha udhibiti wa magonjwa. Mfugaji anapaswa kufuata taratibu zifuatazo katika kulea vifaranga kwa kutumia bruda:-
• Kuweka vifaa vya kuongeza joto kwa mfano taa ya umeme, chemli au jiko la mkaa. Zingatia kiwango cha joto kinachohitajika katika bruda Wiki ya kwanza ni Nyuzi joto 35, wiki ya pili ni nyuzi joto 33, wiki ya tatu ni nyuzi joto 31 na wiki ya nne ni nyuzi joto 29.
• Kuchunguza mtawanyiko wa vifaranga ndani ya bruda ili kutathimini hali ya joto.Wakijikusanya kwenye chanzo cha joto, inaashiria kuwa baridi imezidi hivyo joto liongezwe. Wakiwa mbali na chanzo cha joto maana yake joto limezidi hivyo joto lipunguzwe.
• Bruda iwe na sakafu yenye malalo yatokanayo na maranda ya mbao au pumba za mpunga. Malalo yabadilishwe endapo yataonekana yameloana.
• Bruda iwekwe vifaa vya maji na chakula. Maji na chakula kiwekwe kabla ya kuweka vifaranga.
• Vifaa vya joto viwekwe ndani ya bruda masaa 6 kabla ya kuingiza vifaranga.
• Vifaranga walishwe chakula cha kuanzia gramu 12-15 kwa kipindi cha wiki ya 2. Katika wiki ya 3 wapewe gramu 21-35 kwa kifaranga na chakula hicho kiwepo muda wote.
• Vifaranga wapatiwe vitamin, madini na dawa za kinga (antibiotics); na
• Vifaranga wapatiwe chanjo kulingana na maelekezo ya mtaalamu wa mifugo.Chanjo dhidi ya magonjwa muhimu kwa mfano,Marek’s (mara anapototolewa).
SIKU YA 7-vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDELI).chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kisha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye vitamin.
SIKU YA 14. Wapewe chanjo ya GUMBORO .chanjo hii pia huchanganywa katika maji na kupewe vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu.baada ya hapo vifaranga wepewe vitamin.
Siku ya 21.(wiki ya tatu)Rudia chanjo ya Newcastle.
SIKU 28(mwezi) Rudia chanjo ya GUMBORO.
SIKU 35(mwezi 1 na wiki 1)Kipindi hiki kuku wapewe vitamin ya kutosha.
WIKI YA 6-8 KUKU wapatiwe kinga ya ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi kwa mfugaji asie na utaalam kuwapa kuku,tafta mtaalum kwa kazi hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.
WIKI YA 8 Kuku wapatiwe dawa ya minyoo na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle
Siku ya 21.(wiki ya tatu)Rudia chanjo ya Newcastle.
SIKU 28(mwezi) Rudia chanjo ya GUMBORO.
SIKU 35(mwezi 1 na wiki 1)Kipindi hiki kuku wapewe vitamin ya kutosha.
WIKI YA 6-8 KUKU wapatiwe kinga ya ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi kwa mfugaji asie na utaalam kuwapa kuku,tafta mtaalum kwa kazi hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.
WIKI YA 8 Kuku wapatiwe dawa ya minyoo na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle
Comments